14 Novemba 2016 - 21:28
 Kikundi cha jeshi la kujitolea nchini Iraq chaanza hatua yatatu ya mashambulizi ya kuikomboa Musol + picha

Kwa juhudi za wapiganaji wa wananchi wa Iraq wa kujitolea walio na wivu na nchi yao, ambao waliitikia wito wa kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq, wamefanikiwa kuanza hatua ya tatu ya mashambulizi ya kuukomboa mji wa Musol magharibi mwa mji huo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hatua ya tatu ya mashambulizi ya kuukomboa mji wa Musol yameanza asubuhi ya Jumatatu magharibi mwa Musol.
“Ahmad Al Asadiy” msemaji mkuu wa jeshi la kujitolea la Iraq siku ya Jumatatu amesambaza ujumbe wake na kutangaza kuwa: kwa juhudi za mujahidina na wapiganaji wa kujitolea nchini Iraq ambao ni walinzi wa mipaka ya nchi hiyo, wale ambao waliitika wito wa kukabiliana na magaidi wa Daesh nchini humo, kwa uwezo wa mwenyezi mungu imeanza hatua ya tatu ya mashambulizi ya kuyakumboa maeneo ya Magharibi mwa Musol.
Aidha ameongeza kwa kuwaomba wananchi wa Iraq hususan walioko katika sehemu zinazokaliwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh kusaidina na kushikamana bega kwa bega na majeshi yake katika sehemu za mapambano wanazokwenda kuzikomboa, ili kurahisisha ukomboaji wa sehemu hizo kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh nchini humo.
Naye amesisitiza kuwa jeshi la kujitolea nchini humo litaenda na mapambano mpaka maeneo yote yanayokaliwa na magaidi wa Daesh kukombolewa na kusambaratika kwa kikundi hicho nchini Iraq.
Jeshi la kujitolea nchini Iraq liliopewa mamlaka ya kuyakomboa maeneo ya magharibi ya Musol mpaka sasa yamefanikiwa kuvikomboa vijiji na maeneo mbalimbali katika hatua mbili ziliopita, ambapo sasa imeanza hatua ya tatu.
Mashambulizi ya kuikomboa Musol yalianza 17 mwezi Oktoba mwaka 2016 kwa amri ya (Haidar Al Abadiy) waziri mkuu na ni amirijeshi mkuu wa nchi hiyo, wakishirikiana na majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo na majeshi yakujitolea wananchi nchini humo.
Mji wa Musol ndio makao makuu ya mkoa wa Nineveh ambao ni mkoa unawakazi wengi zaidi baada ya mkoa wa Baghdad ambao pia ni mji wa kibiashara na uchumi nchini humo, ambapo uliingia mikononi mwa magaidi wa Daesh mwaka 2014.

mwisho wa Habari/290